emblem

ARDHI UNIVERSITY

News and Events

Mafunzo Elekezi (Induction) kwa Wafanyakazi Wapya wa Chuo Kikuu Ardhi

Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu ya Chuo Kikuu Ardhi imeendesha Mafunzo kwa Wafanyakazi Wapya wa Chuo Kikuu Ardhi, tarehe 24 Januari, 2023 katika Ukumbi wa IHSS, Chuo Kikuu Ardhi.

Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Evaristo Liwa ambaye aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. John Lupala, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Ally Namangaya pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Anna Mushi.

Mafunzo hayo yalilenga kuwakaribisha watumishi wapya katika Jumuiya ya Chuo Kikuu Ardhi pamoja na kutoa elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Chuo ikiwemo malengo, matarajio na mipango ya muda mrefu na mfupi. Masuala mengine yaliyoelezewa ni pamoja na kukumbushana sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa umma, mafunzo kazini na ujazaji wa fomu za tathmini ya utendaji kazi.